Mutahi Kagwe

Serikali imetangaza mpango wa kununua ngano zaidi kutoka kwa wakulima na kupunguza akiba ya magunia 321,000 iliyosalia kwenye hifadhi zake. Waziri wa Kilimo, Mutahi Kagwe, amesema hatua hii inalenga kusaidia wakulima waliokumbwa na changamoto ya soko la bidhaa zao.

Akizungumza na waandishi wa habari Jumatatu, Waziri Kagwe alisema kuwa kuanzia Jumanne, wakulima wanaweza kupeleka mazao yao kwenye maghala ya Bodi ya Kitaifa ya Nafaka na Mazao (NCPB). Aidha, amewataka wakulima kutozuilia mazao yao kwa zaidi ya juma moja ili kuepuka hasara.


Tangazo hili linajiri siku chache baada ya wakulima wa ngano kutoka Kaunti ya Narok kuandamana wakilalamikia ukosefu wa soko licha ya mavuno mazuri msimu huu. Wakulima hao walidai kuwa kuna watu wenye ushawishi serikalini wanaodhibiti ugavi wa ngano kwa manufaa yao, huku wasagaji wakidaiwa kupewa maagizo ya kununua ngano kutoka kwa kundi maalum kabla ya kununua ile ya wakulima wengine.

 

March 4, 2025