Msemaji wa serikali nchini Dr Isaac Mwaura amesema serikali imejenga zaidi ya masoko elfu moja ya kisasa kote nchini.
Akizungumza alipokuwa akikagua mradi wa ujenzi wa soko la Kisasa katika eneo la Suswa Narok mashariki, Mwaura alishikilia dhamira ya serikali ya kuendelea kujenga masoko ya kisasa ili kuimarisha shuguli za kibiashara kote nchini.
Vilevile Mwaura alitoa changamoto kwa wafanyabiashara kukumbatia Teknologia kwa kuuza bidhaa zao kwa njia ya mitandao ya kijamii.
Kwa upande wao Kina mama katika Soko hilo waliipongeza serikali kwa kuweka vituo mbalimbali ndani ya soko hilo hatua ambayo wanasema itarahisisha biashara zao.