Ibada ya misa ya wafu hii leo iliandaliwa katika kanisa la Holy Family Basilica jijini Nairobi, ili kumuaga na kutoa heshima za mwisho kwa Papa Francis.

Katika homilia yake, mwakilishi wa papa nchini Kenya askofu mkuu Bert Van Megen, aliwahimiza wakristu na haswa viongozi kuiga mfano wa papa wa kuongoza kwa unyenyekevu na bila ubaguzi wowote.

Askofu mkuu Bert pia aliangazia matendo ya Papa ambapo alipenda kutangamana na watu waliokuwa wakiteseka kutokana na changamoto mbalimbali za kimaisha.

Maneno ya askofu mkuu Bert yalitiliwa mkazo na askofu mkuu wa jimbo kuu la Nairobi mhashamu Philip Anyolo ambaye alisifia unyenyekevu wa papa katika uongozi wake.

Kwa upande wao viongozi mbalimbali nchini waliohudhuria ibada hiyo ya misa, wakiwemo rais wa zamani Uhuru Kenyatta na jaji mkuu Martha Koome, walishikilia unyenyekevu wa Papa katika uongozi wake sawa na juhudi zake za kupigania haki na Amani katika mataifa ya ulimwengu.

April 25, 2025

Leave a Comment