Naibu wa Rais Rigathi Gachagua ameahidi kuwa wakenya hawatakua na haja ya kuhofu kuhusu kufurushwa makwao kiholela au kubomolewa makaazi yao nyakati za usiku.
Akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa shule ya Komarok jijini Nairobi alikoandamana na Rais William Ruto, Gachagua amesema kwamba serikali ya Rais William Ruto imetoa ilani kwa viongozi wote watakaotekeleza maagizo yoyote ya kuwafurusha wananchi kutoka kwa makaazi yao pasi na kujadiliana na idara za usalama katika kaunti husika. Naibu wa rais amesisitiza wakenya watakao furushwa kutoka katika ardhi ambayo si yao watapata maeneo mbadala watakapoishi.
SAUTI: Kauli ya Naibu wa Rais Rigathi Gachagua
Katika hafla hiyo aidha, Rais William Ruto aliahidi kuwa wizara ya ardhi imeanzisha juhudi za kutoa zaidi ya hatimiliki 4000 za shamba kwa wakaazi katika kaunti ya Nairobi, kama mojawapo ya njia za kukabiliana na matatizo yanayoibuka kuhusu ardhi katika kaunti hiyo pamoja na kutoa nafasi kwa wananchi kutekeleza miradi ya maendeleo bila hofu.
Soma Pia
- Nyanja za Kilimo November 26, 2024
- CHIMBUKO LA TAMADUNI – JAMII YA MAA November 26, 2024
- CHIMBUKO LA TAMADUNI – JAMII YA ABAGUSII November 26, 2024
- SIKU YA MTOTO WA AFRIKA | Makala November 26, 2024
- Rais William Ruto aagiza kusitishwa kwa kanadarasi iliyotolewa kwa Adani. November 21, 2024