Aliyekuwa mbunge wa Narok Kaskazini Moitalel Ole Kenta amefurahia uamuzi uliotolewa na mahakama kuu ya Narok, ukiidhinisha hatua ya kurufushwa kwa wananchi kutoka katika msitu wa Mau.
Akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya uamuzi huo wa Alhamisi 13.10.2022, Kenta uamuzi huo umepiga muhuri juhudi za wanaharakati wengi waliokuwa wakipigania hadhi ya msitu wa Mau wakiwemo viongozi wa serikali iliyopita kama Vile Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta, aliyekuwa waziri wa misitu na Mazingira Keriako Tobiko pamoja na aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga waliotangaza peupe kuunga mkono kufurushwa kwa wananchi kuoka katika msitu huo.
Katika uamuzi huo uliotolewa kwa kauli moja na majaji watatu ambao ni jaji Muhammad Kulow, Jaji John Mutungi na jaji George Ong,ondo hakuna mtu hata mmoja atakayeruhusiwa kurejea kwenye msitu huo wakiutaja msitu huo kama chemichemi muhimu ya maji katika kaunti ya Narok na hata taifa la Kenya, wakiongeza kuwa kuwa ipo haja ya kuhifadhi mazingira hayo kwa ajili ya vizazi vijavyo. Kesi ya kuwataka wananchi kurejea katika msitu huo iliwasilishwa na wakili Kimutai Bosek kutaka watu waliofuruswa kutoka msitu wa mau kurejea katika msitu huo.
SAUTI: Aliyekuwa mbunge wa Narok Kaskazini Moitalel Ole Kenta.
Kenta pia ametoa changamoto kwa serikali ya sasa ya Kaunti ya Narok kuendeleza juhudi za kuulinda msitu huo, hasa kuweka ua unaofaa ili kusaidia kupunguza mizozano ya mara kwa mara kati ya idara za serikali na wananchi katika maeneo yanayopakana na msitu huo.
Uamuzi huo umeungwa mkono na wakili Martin Kamwaro na Alan Meigati waliowakilisha marafiki wa mau wakisema mahakama hiyo imefanya haki kuamurisha watu wote kuondolewa katika msitu wa mau. Kamwaro amesema uamuzi huo ni wa haki kwa wenyeji wa kaunti ya Narok. Aidha baadhi mawakili katika kesi hiyo wamepinga uamuzi huo na kuahidi kuwa watakata rufaa.