Wabunge katika bunge la kitaifa sasa wanaitaka tume ya huduma za walimu nchini TSC kusitisha zoezi la kuwahamishwa walimu kwa lazima wakisema kuwa waalimu wana haki ya kufanya kazi mahali popote katika taifa hili hata katika maeneo wanayoyotoka.
Wabunge hao walikua wakiijadili hoja ya munge wa Lurambi Titus Khamala ambayo inaitaka tume ya TSC kuangazia upya sera zake za uhamisho na kuwahusisha walimu wenyewe katika shughuli ya uhamisho. Tume ya TSC imewekwa kwenye kurunzi ikitajwa kuhusika na uhamisho wa walimu pasi na kuwahusisha kama washikadau wakuu, jambo ambalo wabunge wanadai kuwa linahitilafiana na maisha ya walimu na hata utendakazi wao.
Sehemu ya wabunge katika vikao vya leo, walionekana kuunga mkono hoja hii wakiitaka TSC kuwaruhusu walimu kufanya kazi hata katika maeneo yao ya nyumbani huku wakidokeza kuwa sera za uhamisho zinazotumiwa na TSC kwa sasa hazina uwazi.