Ili kuwa na kizazi cha siku za usoni, Watoto huwa kiungo muhimu katika kila jamii. Katika jamii ya kimaasai, Watoto walianza kulindwa wakiwa katika tumbo la mama, na hivyo kina mama wajawazito waliangaziwa kwa njia tofauti wakilinganishwa na wanajamii wengine.
Baada ya kujifungua, jamii ya wamaasai ilikua na njia ya kipekee ya kuwakaribisha Watoto katika jamii, mama akihusishwa kwa kiwango kikubwa katika safari ya kwanza ya mwanawe ulimwenguni, hivyo basi, Utunzanji wa mama aliejifungua pia ulitiliwa maanani ili aweze kurejea katika ukamili wake.
Kwa malalamishi yoyote kuhusiana na Makala haya Wasiliana nasi.