Huku zoezi la kusambaza chakula cha msaada likiendelea katika maeneo mbalimbali kaunti ya Narok, onyo imetolewa kwa watu wanaouza chakula hicho kwa wakaazi wa maeneo yanayokabiliwa na baa la njaa. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa shehena ya chakula cha msaada, gavana wa Narok Patrick Ntutu amesema kuwa kuna baadhi ya watu wanaopanga kuuza chakula hicho kwa manufaa yao.
We are all aware of serious climate changes that has occasioned severe drought countrywide exacerbating our food situation. Today, together with the Narok County Commissioner, we have flagged off food relief, donated by the national government to all counties. pic.twitter.com/eGZtoGYOu7
— Governor Patrick Ole Ntutu (@OleNtutuK) October 28, 2022
Ntutu ameeleza kuwa Narok imepokea na kusambaza magunia 3,200 ya kilo 50 za mchele na magunia 1,280 ya kilo 50 za maharage. Chakula hicho kimesambazwa katika maeneobunge ya TransMara magharibi, TransMara mashariki, Emurua Dikir, Narok magharibi, Narok mashariki, Nairagie Enkare, Narok ya kati na Narok kusini.
We have received and distributed 3,200 bags of 50kgs of rice and 1,280 bags of 50kgs of beans. The food has been distributed to Trans Mara west, Trans Mara East, Emurua Dikir, Narok West, Narok East Nairagie Enkare, Narok Central and Narok South; all receiving an equal share
— Governor Patrick Ole Ntutu (@OleNtutuK) October 28, 2022