Marekani imeelezea wasiwasi wake kwamba taifa la Rwanda linawaunga mkono waasi wa kundi la M23 katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na kujiunga na miito ya Umoja wa Mataifa inayotaka amani idumishwe tena.
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani Ned Price amewaambia waandishi habari mjini Washington kwamba msaada wa dola kwa ajili ya makundi yaliyojihami na silaha haukubaliki na wanasisitiza wasiwasi wao kuhusu msaada wa Rwanda kwa M23.
Price amezihimimiza nchi katika ukanda wa afrika mashariki na Kati zishirikiane kurejesha amani, usalama na uaminifu huku zikiheshimu mamlaka na uhuru wa mipaka. Pia amesema maafisa wa Marekani wamekuwa wakiwasiliana mara kwa mara na wenzao wa Rwanda na Congo kuhusu hali ya wasiwasi inayoendelea kuongezeka.