Rais William Ruto amesema kuwa taifa la Kenya limeweka malengo ya kuhakikisha kuwa kuna asilimia 30 ya misitu katika taifa la Kenya ikifikia mwaka wa 2030.
Rais amesema kuwa hili litasaidia taifa la Kenya katika juhudi zake za kukabiliana na mabadiliko ya hali ya anga. Ruto ameyasema haya katika hotuba yake katika kikao cha umoja wa mataifa cha mabadiliko ya hali ya Anga almaarufu COP27 kinachoendelea katika eneo la Sharm El Sheikh katika taifa la Misri.
Rais Ruto aidha ametoa wito wa kushirikiana kati ya mataifa yote ulimwenguni iwapo ndoto ya ulimwengu usio na athari za mabadiliko ya hali ya Anga unafaa kuafikiwa.