Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta amewaomba wapiganaji katika maeneo tofauti ya taifa la Congo DR, kukumbatia njia mbadala za kutatua tofauti zao, na kusitisha mapigano yanayoendelea katika taifa hilo.
Uhuru alikua akizungumza baada ya kuhudhuria kikao cha mashauriano na kutafuta njia za kurejesha amani katika taifa hilo, ameziomba pande zote husika kushirikiana na kutafuta suluhu kwa majadiliano badala ya kuendelea na kuzozana, akiweka bayana kwamba wananchi wa taifa hilo wanaendelea kuumia kutokana na vita hivyo.
Kauli ya Rais Mstaafu inakujia siku kadhaa baada ya wanajeshi wa Kenya kuwasili katika taifa hilo kwa ajili ya kusaidia katika shughuli za kurejesha amani.
Soma zaidi: Kikosi cha kwanza cha wanajeshi wa KDF chaelekea nchini DRC.