BY ISAYA BURUGU 16TH NOV 2022-BAADHI YA viongozi katika kaunti ya narok wamejitokeza kumpongeza aliyekuwa mgombeaji wa kiti cha ugavana narok kupitia chama cha odm moitalel ole kenta kwa kuwasilisha ombi kwenye mahakama kuu ya narok kuondoa kesi aliyowasilisha kwenye mahakama hiyo kupinga ushindi wa gavana wa sasa wa narok patrick ole ntutu aliyechaguliwa kupitia chama cha uda.
Hatua yake Kenta ikijiri kufuatia wito wake askofu wa kanisa la kianglikana Jackson ole Sapit la kuwataka viongozi wote ambao wamewasilisha kesi za kupinga ushindi ya wale waliotangazwa washindi katika uchaguzi mkuu ambao umepita kwenye kaunti za maa kuziondoa kwa ajili ya kuleta umoja na amani ya jamii hiyo.