BY ISAYA BURUGU 8TH DEC 2022-Kamishna wa tume huru ya uchaguzi na mipka nchini IEBC Francis Wanderi amejiuzulu baada yar ais Wiliam Ruto kumsimamisha kazi Pamoja na makamishna wenzake watatu.Wanderi amekuwa kamishna watatu kujiuzulu baada ya Justus Nyangaya na naibu mwenyekiti wa EINC Juliana Cherera.
Kupitia taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya Habari Wanderi amesema uamuzi huo umesabbaishwa na ukosoaji usiofaa ambao anasema umemsababishia fedheha na kutilia shaka maadili yake kuhudumu katika tume hiyo.
Kamishna huyo ameonya dhidi ya uamuzi wake kuchukuliwa kumanisha kuwa amekiri madai yaliyotolewa dhidi yake.Aidha ameonya kuwa iwapo mfumo wa usimamizi wa tume hiyo hautashughulikiwa ipasavyo migogoro itaendelea kushuhudiwa.