BY ISAYA BURUGU 10TH DEC 2022-Msanii mkongwe wa miziki aina ya Rumba kutoka taifa la Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, Tshala Muana ameaga dunia.

Taarifa hizo za tanzia kutoka taifa hilo zilisambazwa kote duniani Usiku wa kuamkia leo ambapo wapenzi wa Rhumba walijumuika mitandaoni kutuma risala za rambi rambi kwa ndugu, jamaa na marafiki wa mama huyo mkongwe. shala Muana alizaliwa mwaka wa 1958 nchini Kongo kama Elizabeth Muidikay.

Alianza kazi yake ya kisanii kama mcheza densi wa bendi ya muziki ya Tsheke Tsheke Love mnamo 1977 kabla ya kugeukia kuimba.

Anajulikana kwa nyimbo kadhaa kama vile Karibu Yangu, Vuluka Dilolo, Chena, Nasi Nabali, Mutuashi miongoni mwa vibao vingine vingi ambavyo vilimwezesha kushinda tuzo nyingi kitaifa na kulipalilia jina lake kama mwanamuziki wa Rhumba wa Kike kutoka taifa hilo lililokuwa chini ya Ukoloni wa Wabelgiji.

 

December 10, 2022