BY ISAYA BURUGU ,12TH DEC 2022-Maafisa wa polisi eneo la Kilimani wamemtia mbaroni jambazi sugu anayeaminika kuwa kiongozi wa genge ambalo limekuwa likijihusisha na visa vya wizi wa kimabavu eneo la kilimani na viungani mwake jijini Nairobi.
Peter Waithaka mwenye umri wa miaka 33 ametia mbaroni eneo la Eastlands baada ya kuandamwa na makachero kw amuda wa saa 48.Katika ripot iliyotolewa na idara ya upepelezi wa jinai DCI, inadokeza kuwa Waithaka nanashukiwa kuwa ndie aliye tekeleza mauaji ya raia mmoja wa ugiriki Alex Marcopaulo, mnamo mwezi Oktoba.
Waithaka anasemekana kumwendea Marcopaulo katika makutano ya barabara ya Menellik-Ngong na watu wengnine wawili na kumwibia bidhaa zake na kumfyatulia risasi na kumjeruhi upande wa kulia wa kifua chake kabla ya kutoroka kutumia pikipiki.
Baadaye Marcopaulo aliaga dunia katika hospitali ya Nairobi Women’s baada ya juhudi za kuokoa Maisha yake kutofanikiwa.DCI inasema Waithaka aliachiliwa hivi maajuzi kutoka jela baada ya kuhudumu miaka sita kwa kosa kama hilo.