Spika wa seneti Amason Jeffa Kingi ameitisha kikao maalum cha bunge hilo hiyo kesho jumanne kutathimini hoja ya kumwondoa mamlakani gavana wa Meru Kawira Mwangaza iliyopitishwa na bunge la kaunti ya meru tarehe 14 mwezi huu wa Disemba.
Kingi kupitia notisi rasmi kwenye gazeti la serikali iliyochapishwa tarehe 16 mwezi huu ametangaza kuwa kikoa hicho kinafuatia ombi kutoka kwa kiongozi wa wengi Aaron Cheruiyot na spika wa bunge la Meru Ayub Bundi kujadili swala hilo.
Kingi ameongeza kuwa kikao hicho kitaandaliwa katika majengo ya bunge la seneti kuanzia saa nane unusu kesho jumane.
Mwangaza aling’atuliwa baada ya wawakilishi wadi 67 wa bunge la Meru kupigia kura hoja ya kung’atuliwa kwake.
Hoja hiyo ilipendekezwa kwa mara ya kwanza na mwakilishi wadi wa Abogeta magharibi Dennis Kiogora tarehe 22 mwezi Novemba.
Wawakilishi wadi hao wanamtuhumu gavana Mwangaza kwa kukiuka katiba na matumizi mabaya ya mamlaka.
On Tuesday 20th December, 2022, The Senate will have a special sitting in the Chamber as from 2.30pm to hear the charges against Hon Kawira Mwangaza, the Governor of Meru, as filed by the County Assembly of Meru. pic.twitter.com/UhAhzUkm9l
— Rt. Hon. Amason Jeffah Kingi, EGH. (@governorkingi) December 17, 2022