Wawakilishi wa Kenya katika bunge la Afrika Mashariki EALA, wametwaa kiapo cha uaminifu na utumishi katika makao makuu ya afrika Mashariki mjini Arusha katika taifa Jirani la Tanzania.
Viongozi hao walikua miongoni mwa wabunge 63 kutoka mataifa saba ya Afrika mashariki waliochaguliwa hivi karibuni, na waliotwaa kiapo cha kutumikia jumuia ya Afrika mashariki kwa kipindi cha miaka 5 ijayo.
Wawakilishi wote tisa wa taifa la Kenya wanaojumuisha Kanini Kega, David Sankok, Winnie Odinga, Kennedy Kalonzo, Hassan Omar, Zipporah Kering, Falhadha Iman Dekow, Godfrey Mwangi Maina na Suleiman Shabbal walihudhuria hafla hiyo.