BY ISAYA BURUGU 20TH DEC 2022-Wizara za uchukuzi na usalama wa ndani zimetangaza kuwa zitaendesha msako kwa Pamoja dhidi ya madereva wanaoendesha magari bila uajibikaji na kusabbaisha ajali msimu huu wa sherehe za krismasi.Kwenye kikao cha Pamoja kwa wanahabari,Waziri wa uchukuzi Kipchumba Murkomen na mwenzake  wa usalama wa ndani Kithure Kindiki wanasema hakuna dereva atakayesazwa iwapo atapatikana akiendesha gari akiwa mlevi au bila kufuata kanuni za barabarani.

Hata hivyo Waziri Murkomen ametangaza kuwa serikali imo mbioni kuweka mipango ya kudumu kukabili wanovuanja sheria za barabarani siku zijazo kwa kuweka  kamera za CCCTV.

Naye Waziri Kindiki amewaonya walio na mazoea ya kugema  pombe haramu misimu ya sherehe inapobisha hodi ili kupata pesa za haraka huku wakihatarisha Maisha ya wananchi kuwa hawatasazwa.

 Wakati huo huo kaunti kamishna kwenye kaunti  zote 47 nchini  maniabu wao,machifu sawa  na maibu wao Pamoja na viongozi wa nyumbani kumi na wazee wa mitaa  wametakiwa kuwa macho wakati huu wa msimu wa sherehe kumkabili mtu yeyote atakayewadhulumu Watoto.

Waziri wa usalama wa ndani Kindiki Kithure amesema kuwa ni katika kipindi kama hiki ambapo visa vyu dhulma za kingono na hata kimwili dhidi ya Watoto huripotiwa kwa wingi kwani wananchi wana safari na kujumuika na jamaa na familia kwa sherehe hizo.Visa hivyo vikiripotiwa manyumbani.

 

 

 

December 20, 2022