Kupitia notisi kwenye gazeti rasmi la serikali iliyochapishwa na rais William Ruto hivi leo jukumu la Kamau jipya linaanza leo na litakamilika katika muda wa miaka mitatu.
Kamau anachukua mahala pa Lewis Nguyai aliyehudumu kwenye wadhifa huo tangu feburuari mwaka jana baada yake kuteuliwa na aliyekuwa rais Uhuru Kenyatta.
Lewis Nguyai alikuwa mbunge wa eneo bunge la Kikuyu.
Rais Ruto pia amemtuea aliyekuwa mkuu wa majeshi Julius Karangi kama mwenyekiti wa bodi ya baraza la kitaifa la idadi na maendeleo .
Aidha Karangi anachukua nafasi ya aliyekuwa wa Kinangop David Ngugi aliyechaguliwa mwezi mei 2021. Karangi atahudumu hadi tarehe 20 mwezi Julai.
Kwingineko rais Ruto amemteua aliyekuwa mgombea wa ugavana wa Nyamira Walter Nyambati kama mwenyekiti wa bodi ya Geothermal Development Company, kwa muda wa miaka mitatu.