Serikal ya kitaifa inapani kuondoa kozi za biashara zinazofunzwa katika taasisi za elimu ya ufundi (Tvet) na badala yake kuongeza kozi za sayansi, teknolojia, uhandisi na hisabati almaarufu (Stem) katika kipindi cha miaka 3 ijayo.
Haya yanajiri huku Rais William Ruto akitangaza mipango ya kuajiri waalimu wapatao 3,000 katika taasisi hizi kufikia mwezi Machi ili kuimarisha kiwango cha masomo kinachotolew akatika taasisi hizi na kukidhi mahitaji ya ulimwengu wa sasa.
Waziri wa elimu nchini Ezekiel Machogu, alitoa mwongozo huu kwa wakuu wa taasisi hizi, akiwataka kukumbatia kozi za STEM akiongeza kwamba mamlaka ya taasisi za TVET imesajili na kudhibitisha zaidi ya taasisi 2,340, wakufunzi 4,604 na programu 11,299 ili kufanikisha masomo katika taasisi hizi.