Mshukiwa wa utapeli kupitia ubadilishaji wa laini za simu Hillary Langat Matindwet almaarufu David Mutai, ameachiliwa kwa dhamana ya shilingi 300,000 baada ya kukana mashtaka dhidi yake.
Mshukiwa huyo alikamatwa mwishoni mwa mwaka jana katika kaunti ya kericho, na amekuwa akizuiliwa katika kituo cha polisi cha Muthaiga, baada ya maafisa wa polisi kupewa kibali cha kumzuia kwa siku mbili zaidi tarehe 3 mwezi huu.
Hapo jana mahakama iliomba kupewa muda Zaidi, ili kutoa uamuzi kamili. Katika kikao cha mahakama hii leo, Hakimu katika mahakama ya Kiambu ameamuru Hillary kuachiliwa huru kwa dhamana hiyo.