Wakulima humu nchini watafaidi pakubwa kutoka kwa serikali ya kitaifa, baada ya serikali kuanzisha mchakato wa kutoa huduma kwa wakulima hawa kwa njia za kidijitali.
Rais William Ruto amesema kwamba teknolojia itaiwezesha serikali kuwaondoa mdalali wanaowahujumu wakulima na kusababisha kuongezeka kwa gharama ya uzalishaji wa chakula. Rais aliyasema haya katika hotuba yake kwenye kikao cha mashauriano kati yake na baraza la mawaziri katika eneo la Nanyuki.
Mpango wa kuwasajili wa kulima kidijitali, utawezesha wakulima hawa kupokea ruzuku na msaada mwingine wa serikali kwa upesi.Rais pia amewaomba mawaziri pamoja na makatibu wakuu, kuendeleza utendakazi wao kwa uwazi, na kutetea maslahi ya wakenya ili kuhakikisha kwamba ndoto ya serikali ya Kenya kwanza ya kuinua maisha ya wakenya inaafikiwa.
Kikao hicho ambacho kilianza siku ya jana, kinatarajiwa kutumiwa na serikali katika kuweka mipango yake ya mwaka huu, na njia mwafaka za kuimarisha uchumi wa taifa.