BY ISAYA BURUGU 11TH JAN,2022-Wakaazi wa eneo la Majengo viungani mwa mji wa Narok wanakadiria hasara ya mamilioni ya fedha kufuatia moto kubwa uliyoteketeza nyumba  moja ya makaazi  eneo hilo usiku wa kuamkia leo.

Wakaazi wanasema Nyumba nne na duka ni baadhi ya zilizoteketea. Wakaazi hao wameilamu idara ya zima moto ya serikali ya kaunti ya Narok kwa kukosa kuajibika ipasavyo katika kukabili Mikasa ya moto ambayo imekuwa ikiripotiwa sehemu mbali mbali za mji katika siku za hivi karibuni.

 Vile vile wakazi hao wameomba gavana wa kaunti ya Narok Patrick Ntutu kuhakikisha gari za zima moto iko imara ili kusuia majanga na kupelekea wengi kupoteza mamilioni ya fedha siku za usoni.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

January 11, 2023