Katika jamii ya kimaasai, mtoto aliyezaliwa hakupewa jina mara moja, kwani shughuli nzima ya kumpa mtoto jina ilikua ni hafla maalum na ambayo ilikua na sheria zake zilizofuatwa.
Katika siku ya kupewa jina kwa mtoto, familia ya mtoto ilitafuta msimamizi wa mwana wao, aliyekuwa wa jinsia moja na mtoto mwenyewe aliyefaa kutoka katika familia au ukoo tofauti na mtoto mwenyewe. Msimamizi huyu alifaa kuwa mtu mwenye maadili mema na aliyekuwa wa kupigiwa mfano na wanajamii wenzake, na ndiye alitekeleza jukumu hili katika hafla iliyojumuisha pia kumchinja kondoo.
Kama tu jamii zingine humu nchini, jamii ya kimaasai ilikua pia na mfumo maalum wa kupeana majina kwa Watoto waliozaliwa, kwani jina lilichukuliwa kama jambo la muhimu katika maisha ya mtoto, ikiaminika kwamba jina lingesaidia mtoto kuwa mtu wa maana katika jamii.
Iwapo una malalamishi yoyote kuhusiana na Makala haya Wasiliana nasi, au uwasiliane na John Waicua kwa barua pepe j.waicua@radioosotua.co.ke