Jukumu la malezi ya Watoto katika tamaduni na jamii ya kimaasai, lilikua jukumu la wanajamii wote, kuanzia kwa wazazi wa mtoto, jamaa wa karibu, Watoto wenzake na hata jamii nzima kwa ujumla. Ili kuhakikisha kuwa mtoto amepokea malezi yanayomfaa, mtoto alipata kuongozwa kwa ushirikiano, akifunzwa yaliyo mema na kuonywa dhidi ya yasiyokubalika katika jamii.
Alipofika umri wa miaka sita, karamu spesheli iliandaliwa ili kumruhusu mtoto kutangamana na Watoto wenzake kutoka katika familia tofauti, akianza kufanya shughuli ndogondogo kama za kuwapelekea mifugo malishoni
Kutokua ma mfumo bayana wa elimu katika tamaduni hii, haikua maana kuwa Watoto hawakupokea mafunzo, badala yake ilikua jukumu la nyanya na wazazi wengine wa kike kutoa mafunzo haya kwa njia ya kusimulia hadithi zilizosheheni mafunzo tele, sawa na nyimbo ambazo zilikua na majukumu ya kuonya, kuelimisha, kufahamisha Pamoja na kuburudisha.
Iwapo una malalamishi yoyote kuhusiana na Makala haya Wasiliana nasi, au uwasiliane na John Waicua kwa barua pepe j.waicua@radioosotua.co.ke