Hafla ya kupashwa tohara katika jamii ya kimaasai, ilikua ya kipekee kwani iliashiria mwanzo mpya kwa kila aliyepita hafla hii. Ngariba akisaidiana na wasimamizi walitekeleza hili katika eneo maalum lililoteuliwa, kabla ya tambiko lililohusisha maziwa na damu, kunyolewa nywele na kubadilisha mavazi kuetekelezwa.
Katika jamii ya kimaasai, hafla yoyote iliyoashiria mwanzo mpya, iliandamana na shughuli za kunyoa nywele na kubadili mavazi, ishara kamili kwamba mmoja amekubali kuyaacha yale ya zamani na kukumbatia Maisha mapya.
Hafla hii ya kupashwa tohara hata hivyo, haikukamilika pasi na kula kiapo kwa wanajamii wapya. Tambiko la kupakwa maziwa liliandamana na kiapo kati ya vijana hawa, kuwa wataitetea jamii na kuwalinda mifugo wao didi ya lolote lile.
Iwapo una malalamishi yoyote kuhusiana na Makala haya Wasiliana nasi, au uwasiliane na John Waicua kwa barua pepe j.waicua@radioosotua.co.ke