BY ISAYA BURUGU  12TH JAN 2022-Rais Wiliamu Ruto amekita kambi kwa siku ya pili mfulilizo hivi leo katika chou cha utoaji mafunzo kwa polisi wa utawala cha Embakasi kuongoza hafla ya kufuzu kwa makurutu wa GSU.Hiyo jana rais alikuwa katika chou hicho kuongoza hafla ya kufuzu kwa makurutu wa polisi wa utawala.

Maafisa waliofuzu leo ni 991.Rais akizungumza amewataka wawe mfano bora katika kila wafanyalo bali na kuahidi kubboresha mazingira yao ya utenda kazi kwa kuwapa makao bora na huduma za matibbau.Pia amewataka kuzingatia kanuni za kisheria wanapotekeleza majukumu yao ya kulihudumia taifa

.

Waliozungza pia ni Pamoja na Waziri wa usalama wa ndani Kithure Kindiki ambaye amewataka maafisa hao kutekeleza majukuu yao wakikumbuka kuwa taifa linawategemea .

Itakumbukwa kuwa sherehe hizo za kufuzu zimejiri wakati taiafa linakumbwa na changamoto mbali mbali za kiusalama ikiwa ni ishara ya serikali kujitolea kukabili tatizo hilo.

 

January 12, 2023