BY ISAYA BURUGU 13TH JAN 2023-Wakulima katika kaunti ya Narok wamenufaika na mafunzo yanayolenga kuwawezesha kufahamu jinsi ya kuendesha shughuli zao na kupata faida wakati huu taifa linaposhuhudia adhari za mabadiliko ya hali ya hewa.Katika mafunzo hayo yaliyoandaliwa katika shamba la Purko Narok kaskazini ,mashirika mbali mbali ya kilimo yalionyesha bidhaa zao na mbinu ya kustawisha kilimo cha mazao tofauti.
Wakulima walipata mafunzo kuhusu jinsi ya kuendesha kilimo endelevu kwa kutumia mbinu za kisasa sawa na mbegu zinazofanya vyema katika sehemu hiyo.Hafla hiyo iliongozwa na Waziri wa kilimo katika kaunti ya Narok Joyce Keshe. Akizunggumza kwenye hafla hiyo bi Keshe amesifia hatua hiyo anayosema itawafaa wakulima kwa kuwapa mafuzno hitajika.
. Aidha amewataka wanawake katika kaunti ya Narok kuchukulia kilimo kwa makini akisema kuwa watapata usaidizi hitajika kutoka kwa serikali ya kaunti.
Kwa upande wake mkuu wa kitengo cha kilimo bishara katika kampuni ya KBL amesema kampuni hiyo imejitosa katika ufumbuzi wa mbegu za hali ya juu na utoaji mafuzno kwa wakulima ili kuwawezesha kunufaika na shughuli zao za kilimo.
Katika hafla hiyo kampuni ya KBL na washirika wengine walitoa miche 2000 ya miti itakayopandwa katika eneo hilo katika juhudi za kukabili adhari za mabadiliko ya hali ya hewa.