BY ISAYA BURUGU 19TH JAN 2023-Familia ya mwanamke wa miaka 18 aliyeuawa na mwili wake kupatikana bila kichwa katika kichaka cha Rore huko Tigania kaunti ya Meru inalilia haki.
Kwa mjibu wa nyanyake Beatrice Gatwiri msichana huyo aliondoka nyumbani baada ya kukamilisha mtihani wake wa KCSE mwaka jana Kwenda kuishi na mchumba wake kabla ya tukio hilo.
Polisi wanasema msichana huyo alitoweka nyumbani kwa mvulana huyo siku tatu kabla ya mwili wake kupatikana. Ripoti ya polisi inashiria mwili huo haukuwa na nguo za nguo zake za ndani zilikuwa kando ya mwili huo.Familia inasema haiwezi kuzikwa mwili bila kichwa.