BY ISAYA BURUGU,31ST JAN,2023-Washukiwa watatu wa wizi wakimabavu wamekamatwa usiku wa kuamkia leo baada ya maafisa wa polisi kuwapata na bidhaa za kielktroniki zilizoibiwa katika mtaa wa Githurai 44 kaunti ya Nairobi.Washukiwa hao,Francis Itaru, Joel Njoroge na John Warui walikamatwa baada ya maafisa wa polisi kutoka kituo cha polisi cha Kasarani kupashwa Habari.
Taarifa kutoka idara ya upelelezi wa jinai DCI aidha imeongeza kuwa maafisa wa polisi walikuwa wamefahamishwa kuhusu magari mawili ambayo yamekuwa yakibeba bidhaa za kielektroniki ambazo baadaye huuziwa wafanyibiashara katika eneo hilo.
Watatu hao wamepatikana wakiwauzia wachuuzi bidhaa za kielektroniki na msako wa haraka ukaendeshwa katika gari lao ambapo nambari bandia za usajili wa magari ,funguo kadhaa,kipakatalishi na vifaa vya kuvunja nyumba vilipatikana.
Kwa sasa washukiwa hao wanazuiliwa katika kituo cha polisi cha Kasarani wakisubiri kufikishwa mahakamani.