Chama cha KANU kimetangaza kuwa kimeamtimu aliyekuwa katibu mkuu wa chama hicho Nick Salat kutoka kwa wadhifa huo, kwa kile kilichotajwa kama kukiuka mwongozo wa maadili ya chama.
Katika waraka uliochapishwa na chama cha KANU kupitia mkurugenzi wa mawasiliano katika chama hicho Bw. Joseph Towett, wanachama wa halmashauri kuu ya kitaifa ya chama hicho walikubaliana na pendekezo la kamati ya kinidhamu, iliyopendekeza kubanduliwa kwa Salat kama katibu wa chama.
Mwenyekiti wa kitaifa wa KANU Gideon Moi anatarajiwa kutangaza katibu mpya wa chama hicho katika siku za usoni.