BY ISAYA BURUGU ,16TH FEB,2023-Wito umetolewa kwa Wanafunzi katika shule mbali mbali eneo la Narok Kusini kujitahidi na kuanya bidi katika masomo yao ili waweze kuandikisha matokeo bora.Wito huu umetolewa na mkurugenzi wa elimu eneo la Narok kusini Sankale Ole Sendero .
Akizungumza eneo la Sogoo Narok kusini Sankale amewataka wanafunzi kutilia manani maswala ya elimu baada ya eneo hilo kuzalia nyuma katika maswala elimu kwa muda mrefu.Sankale amesema swala la mimba za mapema imechagia kudorora kwa elimu eneo hilo.
Sankale ametoa wito kwa wanafunzi kuwa wavumilivu maishani na kuwatii walimu pamoja na wazazi wao.Wakati huo huo mkurugenzi huyo wa elimu amewataka wanasiasa kutoingiza siasa mashuleni eneo la Narok.
Sankale amesema baadhi ya wanasiasa wameingiza maswala ya kisiasa shuleni hatua ambayo imepelekea shule nyingi kuandikisha matokeo duni.
Vile vile mkurugenzi huyo wa elimu amewataka walimu na wazazi kushirikiana ili kuzuia dau la elimu kuyumba kaunti ndogo ya Narok kusini.