Kamishna wa tume huru ya uchaguzi na mipika nchini IEBC aliyesimamishwa kazi Irene Masit hivi leo amehudhuria kikao cha mwisho cha kujitetea mbele ya jopokazi lililobuniwa na rais Wiliam Ruto kuchunguza matukio yaliyojiri tarehe 15 mwezi Agosti mwaka jana wakati wa kutangazwa kwa matokeo ya kura za urais.
Masit ni mmoja kati ya makamishna wannne wakiongozwa na naibu mwenyekiti Juliana Cherera waliosimamishwa kazi kutokana na matukio hayo.
Hata hivyo cherera na makamishna wengine wawili walijiuzulu pindi baada ya jopo hilo kubuniwa.Masit kupitia wakili wake Donald Kipkorir aliliambia jopokazi hilo linaloongozwa na jaji mstaafu Agrey Muchelule kuwa yeye hakuwa na hatia kwani alikuwa anafuata maagizo kutoka kwa naibu mwenyekiti baada ya hali kuwa bayana kuwa viongozi wa tume hiyo wakiwemo makamishna walikuwa wamegawanyika.
Vilevile ameikosoa jopokazi hilo kwa kutofuata sheria kikamilifu katika utendkazi wake.