Katika jamii ya Wamasai, morani au Morans hurejelea vijana ambao wamepitia desturi ya kutoka ujana hadi utu uzima. Hii ni hatua muhimu katika utamaduni wa Wamasai, na inahusisha msururu wa mambo kama vile kupashwa tohara, kujitenga na jamii, na pia kupokea mafunzo na maarifa yanayohitajika ili kuwa mtu mzima na shujaa anayewajibika katika jamii. Kwa mujibu wa Mwalimu Joseph Ole Mpaira ambaye amekuwa akituelekeza katika safari hii, kipindi hiki kilikuwa muhimu sana, kwani kilimsaidia moja kupata mafunzo muhimu ya kuwa mwanajamii kamili.

Kinyume na vile wengi wanavyowatambua morani kama watu wa kuzua rabsha na kuhangaisha wanajamii wengine, Maisha yao yaliongozwa na kanuni kali za maadili, wakiwa na mambo kadhaa ambayo yalikuwa mwiko au enturuj kwa kimaasai. Baadhi ya mambo ambayo Morani wa kimaasai hakuruhusiwa kufanya ni pamoja na kula huku akiangwaliwa na kina mama, kutembea pekee yake au hata kujitenga na kundi la wenzake. Mzee mpaira anaendelea kutueleza.

Iwapo una malalamishi yoyote kuhusiana na Makala haya Wasiliana nasi, au uwasiliane na John Waicua kwa barua pepe j.waicua@radioosotua.co.ke

February 22, 2023

Leave a Comment