Baada ya kukamilisha kipindi cha kuwa Morani, vijana hawa sasa walipata nafasi ya kupata mke na kuanzisha familia, pasi na kuangazia hadhi yake, kwani wanajamii wa kimaasi waliamini kwamba kupata mke mzuri ilikuwa baraka kutoka kwa Mungu na pia bahati ya mtu mwenyewe. Hii inamaana kuwa hata yule ambaye alionekana kama maskini Zaidi alikuwa na nafasi sawa ya kupata mke na kuanzisha Familia.
Kulikua na njia mbalimbali za kupata mke kati ya wanajamii hawa. Baadhi ya wanaume waliochukuliwa kama mashujaa walikua na nafasi rahisi kwani wazazi wengine waliwaleta wana wao ili waolewe na shujaa huyu. Wazazi wengine pia walijishughulisha kwa kiwango kikubwa katika kuwatafutia wana wao wake.
Kabla ya kuanzisha familia, uchunguzi wa kina ulitekelezwa ili kuhakikisha kwamba mke ambaye analetwa katika jamii, hana uhusiano wowote wa kiukoo na familia yenyewe, na pia kuhakikisha kwamba jamii aliyotoka ilikuwa inaishi maisha ya kuridisha kwani iliaminika kuwa kumleta mke kutoka katika jamii ambayo ilijihusisha na mambo mabaya kungehitilafiana na uwezo wa familia ile kuimarika.
Iwapo una malalamishi yoyote kuhusiana na Makala haya Wasiliana nasi, au uwasiliane na John Waicua kwa barua pepe j.waicua@radioosotua.co.ke