BY ISAYA BURUGU,4TH MARCH,2023-Mtu mmoja amefariki baada ya kugongwa na gari eneo la Kiangwaci kwenye barabara kuu ya Sagana-Karatina katika eneo bunge la Ndia,kaunti ya Kirinyaga. Wenyeji wameawambia wandishi Habari kuwa marehemu alikuwa ndio manzo anajiandaa kupanda gari wakati alipogongwa na gari.
Wakati huo huo wenyeji wamelalama kuhusu visa vinavyozidi kuongezeka vya ajali za barabarani katika barabara hiyo yenye shughuli nyini.
Wamemtaka mwanakandarasi aliyepewa jukumu la kukarabati barabara hiyo kuweka mabango yanayoonya watumizi wa barabara hiyo ili kuzuia visa kama hivyo .
Mwili wa Mwenda zake umepelekwa katika hifadhi ya maiti iliko karibu huku gari lenyewe likipelekwa kiuo cha polisi cha Sagana.