BY ISAYA BURUGU,9TH MARCH 2023-Mkuu wa mawaziri Musalia Mudavadi amewataka wananchi kusalia watulivu na kuipa serikali ya Kenya kwanza muda wa kutosha kurekebisha hali ya kiuchumi nchini.Akizungumza kwenye mkutano wa mazungumzo na wananchi jijini Nairobi,Mudavadi amesema kuwa Hapana suluhisho la haraka kwa hali ya kiuchumi inayokumba kenya kwa sasa
.Ameongeza kuwa mapigano na vita vinavyokumba Ukraine yameadhiri uchumi wa mataifa mengi duniani kenya ikiwemo.Mudavadi akikosoa upinzani kwa mandamano dhidi ya serikali baada ya upinzani kudai kuwa serikali imeshindwa kukabili hali ngumu ya kiuchumi inayokumba nchi
..Mkuu wa mawaziri akisema kuwa ni sera mwafaka zitakazosaidia kuafiakia lengo la kuboresha hali ya kimaisha ya kila mkenya .