BY ISAYA BURUGU  1ST MAY,2023-Afisa mmoja wa polisi anauguza majeraha ya risasi katika hospitali ya rufaa ya Marsabit baada ya gari la polisi walimokuwa wameabiri kuvamiwa na majambazi katika eneo la kambinye eneo bunge la Laisamis kaunti ya Marsabit .

Wakati wa uvamizi huo maafisa sita wa polisi walikuwa wameabiri gari hilo aina ya Toyota landcruser.Kulingana na idara ya polisi majeruhi ni dereva wa gari la polisi iliyekuwa amekwenda kuwachukua wenzake waliokuwa kazini katika eneo la kambinye.

Ripoti za polisi zimedokeza kuwa majambazi hao walivamia gari hilo barabarani na ndiposa ufyatulianaji risasi ukazuka huku majeruhi akipata majearaha ya tumbo,kifua na kwenye kiuno.

Maafisa hao waliokolewa na wenzao katika kituo cha polisi cha Kambinye.Majeruhi yuko katika hali dhabiti ya kiafya wakati msako umeanzishwa kuwanasa majambazi waliotoroka.

 

 

May 1, 2023