BY ISAYA BURUGU,3RD FEB 2023-Fredrick ole Leliman, afisa wa polisi anayeaminika kupanga mauaji ya wakili Willie Kimani, mteja wake Josephat Mwenda na mwendesha texi Joseph Muiruri mwaka 2016 amehukumiwa kifo.Waliokuwa wafanyikazi wenzake na watuhumiwa Stephen Cheburet Morogo na Sylvia Wanjohi ambao pia walipatikana na hatia ya mauaji wamehukumiwa kifungo cha miaka 30 na 24 mtawalia.
Wakati huo huo aliyekuwa akiwapasha Habari na kufanikisha mauaji hayo ya watu watatu amehukumiwa kifungo cha miaka 20 jela.
Akitoa hukumu hiyo jaji Jessie Lessit amesema mauaji ya wakili Willie Kimani, Mteja wake Josephat Mwenda na dereva Joseph Muiruri kilikuwa kitendo cha kinyama ambacho hakipaswi kushudiwa kamwe .Watuhumiwa wana siku 14 kukata rufaa.
Wakili Willie Kimani, mteja wake Mwenda na mwendesha texi walitekwa nyara walipokuwa wakitoka kataiaka mahakama ya Mavoko kaunti ya Machakos mnamo tarehe 23 mwezi Juni mwaka 2016 ambapo Mwenda alikuwa amewasilisha kesi dhidi ya afisa wa polisi.