BY ISAYA BURUGU,28TH SEPT,2023-Wito umetolewa kina mama sawa na madaktari katika kaunti ya Narok na kote nchini kushirikiana kukomesha dhuluma kwa kina mama wanapojifungua.wito huu umetolewa na kina mama na madaktari kwENYE warsha iliyoandaliwa na shirika la White Rippon Allance Kenya ili kutoa hamasa kwa jamii hasa kwa kina mama wanapotembelea mahospitali .Esther Sadera ni mmoja kati ya kina mama wachanga ambao wamekuwa na hofu ya kutembelea mahospitali wanapojifungua.
Akizungumza na wandishi wa habari afisa wa shirika la White Rippon Allance Kenya Stephen Paan amesema wamefanya warsha ya kuwahamasisha kina mama na umuhimu ya kutembelea hospitali wakiwa na mimba ili kuelekezwa na madaktari.
Kauli yake imeungwa mkono na daktari wa afya katika hospitali ya Ololulunga Narok kusini ambaye amewataka kina mama kaunti ya Narok kuwa wajasiri wanapotembelea mahospitali ili kusuia maafa wanaponifungua na kumshukuru shirika hilo la White Rippon Allance kwa kushirikiana na mafisa wa afya.
Toroitich Chesang ni mhudumu wa kuwasaidia kina mama kujifungua na amesema tayari kina mama wengi wamekuwa wakitembelea mahospitali kupata huduma wanapojifungua. Kina mama wengi mara nyingi wamehofia kutembelea hospitali wakiwa wajawazito wakihofia kudhulumiwa na wahudumu wa hospitali.