BY ISAYA BURUGU,8TH MARCH,2023-Huku Kenya ikiungana na ulimwengu kuadhimisha siku ya Akina mama duniani leo,akina mama katika kaunti hii ya Narok wameitaka serikali kuwasaidia katika kuwapiga jeki kiuchumi kwa kuinua biashara zao ndogo ndogo.
Kwa mjibu wa Sila Letiet ambaye ni mama, kina mama wengi wamekosa kujiendeleza kimaisha kwani hawana fedha za kustawisha biashara zao licha ya kuwa wengi wao ni wenye bidi.Sila amesema serikali ya kaunti na ile ya kitaifa zina nafasi ya kuwakwamua kina mama kutoka lindi la umaskini.
Kauli yake imeungwa mkono na Shantel Naimadu ambaye anasema kina mama ni mashujaa na kuwataka kina mama wachanga kuvumilia changamoto za maisha kwa kufanya bidii maishani.
Samato kamamia anatoa wito kwa kina mama wachanga kuwalea watoto wao kwa madhili mema.Samato amesema kuna changamoto ya maadili katika familia na kina mama ndio wenye uwezo wa kubadilisha jamii.