By Isaya Burugu ,Oct 15,2022-Rais William Ruto amemteua Amin Mohamed Ibrahim kama mkurugenzi mkuu wa idara ya upelelezi wa jinai nchini DCI.Uteuzi huo umechapishwa kwenye notisi katika gazeti rasmi la serikali ya hiyo jana.
Kabla ya uteuzi huo Ibrahim alikuwa akiongoza kitengo cha maswala ya ndani na pia alikuwa amehudumu kwenye nyadhifa mbali mbali ikiwemo kuongoza kitengo cha uchunguzi wa makosa ya jinai yaani CID na kile cha uhalifu wa benki kati ya nyadhifa zingine kuu.
Tume ya kitaifa ya huduma kwa polisi ilikuwa imewaorodhesha watu 10 waliokuwa wametuma maombi ya kutaka wadhifa huo uliyowachwa wazi kufuatia kujiuzulu kwa George Kinoti kama mkurugenzi mkuu wa DCI .
Mnamo jumanne juma hili kumi hao walifika mbele ya jopo la mahiojiano yaliyoendeshwa katika taasisi ya mafunzo ya serikali iliyoko Kabete kaunti ya Kiambu.
Wengine walioorodheshwa ni , Bernard Barasa Walumoli, Eliud Kipkoech Lagat, Gideon Nyale Munga, Esther Chepkosgei Seroney na David Kipkosgey Birech.Wengine walikuwa Jonyo Michael Wiso, Nicholas Ireri Kamwende, Paul Jimmie Ndambuki na Dakta . Simon Mwangi Wanderi.