Aliyekuwa Mgombea wa kiti cha ugavana katika kaunti ya Kirinyaga katika uchaguzi wa Agosti 9 Wangui Ngirici, ameondoa kesi aliyowasilisha mahakamani kupinga ushindi wa Gavana Anne Waiguru. Katika taarifa yake kutangaza uamuzi huo, mwanasiasa huyo amesema aliafikia uamuzi huo baada ya kuichunguza nafsi yake pamoja kusikiliza ushauri kutoka kwa wandani wake, na hivyo kuamua kuiondoa kesi hiyo ambayo inaonekana kama inayoangazia maswala yake ya binafsi badala ya matakwa ya wananchi wa kaunti ya Kirinyaga.
Nimeamua kuchukua uamuzi huu wa kijasiri, ambao hautanifaidi mimi binafsi wala kuhitilafiana na utendakazi wa gavana (Ann Waiguru) bali ni uamuzi ambayo utawafaa watu wa Kirinyaga kikamilifu.
Kwa hivyo nimewaagiza mawakili wangu kuiondoa kesi yangu dhidi ya gavana waiguru mahakamani.
I have decided to take a bold step; One that does not serve to advantage me or disorganise and disenfranchise the Governor but one that serves full advantage to the people of Kirinyaga .
— Wangui Ngirici (@WanguiNgirici) October 5, 2022
I therefore have instructed my lawyers to withdraw my petition against GVN waiguru
Ngirici ambaye alihudumu kama mwakilishi wa kina mama katika kaunti hiyo, ameongeza kuwa licha ya kuwa na ushahidi wa kutosha, ameamua kuchukua uamuzi huo ili kuwaruhusu wananchi wa kaunti ya Kirinyaga kupokea huduma bila kutatizwa, hasa baada ya gavana Anne Waiguru kuchaguliwa kama mwenyekiti wa baraza la magavana nchini. Wakizungumza baada ya kikao cha mahakama, mawakili wa pande zote mbili wameeleza imani yao kuwa ombi la kuondolewa kwa kesi hiyo litakubalika ili kutoa fursa kwa gavana Ann Waiguru kutekeleza majukumu yake inavyofaa.
SOMA PIA
- Magavana Wataka Kufutwa kwa Agizo la Kusitisha Utoaji wa Basari za Wanafunzi January 21, 2025
- Mtu mmoja aaga dunia baada ya kupigwa risasi katika eneo la duka moja, Suswa.. January 17, 2025
- Abiria Wakesha Barabarani Baada ya Wafugaji Kufunga Barabara eneo la Suswa. January 17, 2025
- Maambukizi ya Virusi vya UKIMWI Yapungua kwa Asilimia Kubwa Narok. January 14, 2025
- Mawaziri Wateule Mutahi Kagwe, William Kabogo na Lee Kinyanjui Kupigwa Msasa January 14, 2025