Mgombea wa uenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) Anne Amadi amejitetea kutokana na madai ya kuhusika katika kashfa ya dhahabu.

Katika kesi hiyo, Bruton Gold Trading LLC ilidai kuwa washtakiwa, kwa niaba ya kampuni ya uwakili ya Amadi and Associates Advocates, walipata kinyume cha sheria zaidi ya Ksh.89 milioni kwa dhahabu ambayo hawakuwahi kutoa.

Wakati wa kuhojiwa kwake na jopo la uteuzi wa IEBC mnamo Jumatatu, Amadi aliyekuwa Msajili Mkuu wa Mahakama alisema kuwa alijiuzulu kutoka kwa kampuni hiyo ya mawakili iliyoshtakiwa, mwaka wa 2014 na hana uhusiano wowote na kashfa hiyo.

Aidha Amadi alibainisha kuwa uamuzi wa mahakama uligundua kuwa alihusishwa na kashfa hiyo ila hakuwa na hatia.

Wengine waliohojiwa ni pamoja na Abdulqadir Lorot Ramadhan na Charles Ayako Nyachae.

March 24, 2025

Leave a Comment