BY ISAYA BURUGU 2ND FEB,2023-Ripoti ya kitaifa kuhusu ugonjwa wa saratani iliyozinduliwa leo jijini Nairobi imebainisha kuwa asilimia 46 ya visa vya ugonjwa huo hugunduliwa vikiwa kwenye hatua ya mwisho huku visa vya saratani miongoni mwa Watoto walio na umri wa chini ya miaka 18 vikiwa asilimia mbili .Kaunti za Nakuru na Nairobi ndizo zilizo na idadi ya juu Zaidi ya saratani.
Vilevile asilimia 25 ya visa vya ugonjwa huo nchini vinapatikana kwa walio na umri wa mwaka mmoja hadi 29 ambapo asilimia 75 ya visa huadhiri wakenya walio na umri wa kati ya miaka 30 hadi 84.Visa vya saratani ya matiti miongoni mwa wanawake vimefikia asilimia 26.5 huku saratani ya kizazi ikiwa ya pili kwa asilimia 23.2 ikifuatiwa na saratani ya utumbo kwa asilimia 8.8.
Saratani ya njia ya mkojo kwa wanaume ni asilimia 23.7 huku ile ya koo na utumbo zikifuata kwa asilimia 15.9 na 8.8 mtawalia.
Katika kikao hicho imeabainika kuwa Zaidi ya kaunti ishirini nchini hazina uwezo wa kugundua na kutibu saratani.Gavana wa Tharaka Nithi Muthomi Njuki aliyewakilisha baraza la magavana pia anasema kuna haj aya kuongeza mgao wa fedha unaotengewa vita dhidi ya Saratani.