BY ISAYA BURUGU 15TH NOV,2022-Ripoti iliyozinduliwa na taasisi ya kitaifa kuhusu saratani imefichua kuwa wagonjwa wawili kati ya watatu wanaogunduliwa na ugonjwa wa saratani wako na uwezekano mkubwa wa kuaga dunia kutokana na ugonjwa huo. Kwa mjibu wa taasisi hiyo ,asilimia 70 ya wagonjwa wanaogunduliwa kuwa na saratani wakiwa wamechelewa wana uwezekano wa hali ya juu kuaga dunia.
Kaimu mkurugenzi wa taaisi hiyo Dakta Alfred Karagu amesema juhudi zote zinapaswa kuelekezwa katika utoaji hamazisho kwa umma kuhusu haja ya kusaka matibabu mapema sawa na uchunguzi wa mara kwa mara.
Humu nchini vituo vya matibabu ya saratani vipatavyo 60 vimeidhinishwa kwenye kaunti 16.
Wakatti wa mkutano kuhusu saratani uliyoandaliwa jijini Nairobi leo,mkurugenzi wa hazina yakimatibabu ya NHIF Dakta Peter Kamunyo amesema hazina hiyo imewashughulikia wagonjwa alfu 47 wa saratani katika kipindi cha mwaka jana.