BY ISAYA BURUGU 17TH JULY 2023-Askofu  Gilbert Deya sasa yuko huru baada ya mahakama kuu jijini Nairobi kumwachilia kutokana na makosa yote Matano yanayohusiana na wizi wawatoto yaliyokuwa yakimkabili.

Mahakama imetoa uamuzi kuwa upande wa mashtaka ulikosa kuwasilisha ushidi wakutosha kudhibitisha kesi yake dhidi ya mhubiri huyo.

Mnamo tarehe 4 mwezi Agosti mwaka 2017,Deya alirejeshwa humu nchini kutoka wingereza ili kukabiliana na mashataka ya wizi wawatoto.Katika kesi hiyo,Deya alikuwa ameshatakiwa kwa makosa Matano ya kuiba Watoto watano wote waliokuwa na chini ya umri wa miaka 14 kati ya mwaka 2002 na mwaka 2004 katika mtaa wa  Mountain View Estate jijini  Nairobi.

Mkewe pia alishatakiwa kuhusiana na kuiba Watoto lakini baadaye aliachiliwa huru.

Akizungumza na wandishi Habari baada ya kuachiliwa kwake,Deya amesema amewasamehe waliompitishia mateso hayo  na kusema kuwa anarejea wingereza kuendeleza kazi yake ya kuhubiri.

 

 

 

 

July 17, 2023