Askofu wa jimbo katoliki la Ngong’ John Oballa Owaa hii leo amezindua rasmi kampeni ya kipindi cha kwaresma ya jimbo katika kathedrali ya Mt. Yosefu mjini Ngong’.

Askofu Oballa akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hii, amewahimiza wakristu kuzingatia haki za watu wasiojiweza katika jamii huku akisisitiza umuhimu wa maudhui yam waka huu na kusema kuwa Taifa hujengwa na watu waadilifu.

Aidha Askofu Oballa ametoa wito kwa serikali kuwashirikisha wakenya kikamilifu kwenye masuala ya uundaji sheria kabla ya kuwasilisha miswada bungeni.

Kuhusu suala la gharama ya maisha na ushuru unaotozwa wakenya, Askofu Oballa ameihimiza serikali kuweka wazi matumizi ya ushuru huo kama njia mojawapo ya kuzingatia uadilifu na uwajibikaji.

February 14, 2024