Katibu mkuu wa muungano wa vyama vya wafanyakazi Francis Atwoli ameunga mkono pendekezo la rais William Ruto la kuongeza malipo ya NSSF kutoka Ksh.200 ya sasa hadi 6%. Hii ina maana kwamba wafanyakazi watakuwa wanakatwa 6% ya mishahara yao ya kila mwezi.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari, Atwoli ametoa wito kwa Wakenya kukumbatia kikamilifu kiwango cha 6% akidai kuwa kitawafaidi wafanyakazi wanapostaafu. Atwoli ameongeza kuwa pendekezo hilo limepuuzwa kwa muda mrefu.

Katika mpango wake wa kuwa na ujumuishaji wa sekta isiyo rasmi kama wachangiaji wa hiari , Rais Ruto alisema kuwa shilingi 200 ni kidogo sana kumfaidi mtu yeyote katika uzee wao.

Aidha Pendekezo hilo halijapokelewa vyema na wakenya wengi wakidai kwamba watakuwa na mzigo zaidi wanapolipwa kutokana na nyakati ngumu za kiuchumi.

 

November 1, 2022