BY ISAYA BURUGU,21ST MARCH,2023-Kinara wa Azimio la Umoja Raila Odinga ametangaza kuwa mungano huo utandaa mandamano siku mbili kwa wiki kuaznia wiki ijayo.Kwenye mkutano na wandishi habari jijiini Nairobi hivi leo,Odinga aliyeandamana na kinara wa Wiper Kalonzo Musyoka,Martha Karua wa Narc Kenya, Eugine Wamalwa na katibu mkuu wa chama cha Jubilee Jeremiah Kioni,amesema kuwa mungano huo utakuwa unandaa mandamano kila siku ya jumatatu na Alahamsi kuanzia wiki ijayo.Kupitia taarifa,Odinga amewalaumu maafisa wa polisi kwa kuwachokoza wandamanaji wa Azimio waliokuwa na amani na waliodumisha utulivu wakati wa mandamano yao ya siku ya Jumatatu.
Odinga amesema ni kupitia vitendo hivyo vya polisi ambapo mwanafuzni wa chuo kikuu cha maseno alifariki na watu wengine kujeruhiwa.Odinga pia amefichua kuwa maafisa wa polisi walinuia kumwangamiza yeye na kinara wa Wiper Kalonzo Myoka baada ya magari yao kumiminiwa risasi wakati wa mandamano,hata ingawa wanashukuru kwani hawakuadhirika.
Odinga aidha ameikashfu serikali kwa kutumia polisi visivyo kuwahujumu wandamanaji waliokuwa na amani badala ya kuelekeza mashambulizi hayo kwa magaidi wanaowahangaisha wakaazi wa maeneo ya bonde la ufa.Odinga pia ameagiza kuachiliwa mara moja kwa wafausi wao waliokamatwa jumatatu wakati wa mandamano hayo.
Odinga pia ametangaza kuwa wanapanga kumfungulia mashataka nje na ndani ya nchi kamanda wa polisi wa Nairobi Adamson Bungei kwa ukatili alionyesha.
Katika kikao hicho,Odinga amewatangazia wafausi wao kote nchini kususia bidhaa za kampuni mbali mbali alilosema zinatumiwa kuwahujumu.Bidhaa hizo ni kampuni ya huduma za simu ya safaricom,gazeti la the star la kampuni ya radio African group kati ya zingine.
on